MABADILIKO YA MTAALA(MTAALA ULIOBORESHWA)
MUUNDO WA ELIMU-SEKONDARI YA CHINI
(A flexible education system).
Elimu ya sekondari itagawanyika katika mikondo miwili ambayo ni:
- mkondo wa jumla
- mkondo wa Amali

1.MKONDO WA JUMLA
- Utekelezaji utaanza Januari, 2025.
- Mkondo wa Elimu ya Jumla umejikita kwenye masomo ya kitaaluma.
- Mkondo huu una michepuo 11 ambayo ni: Sayansi, Kilimo, Michezo, TEHAMA, Biashara, Muziki, Sayansi ya Jamii, Sanaa, Upishi, Ushoni na Lugha.
- mkondo wa jumla utahusisha masomo sita (6) ya lazima na masomo ya fani atakayochagua mwanafunzi katika michepuo 11 iliyo tajwa hapo juu
- Masomo sita (6) ambayo ni:-
- kiingereza(English)
- Kiswahili
- Geografia(Geography)
- Historia ya Tanzania na maadili
- Hisabati(B/maths)
- Elimu ya biashara(business study)
- Angalia jedwali hapo chini

MKONDO WA AMALI
- Mkondo huu unaruhusu unyumbufu utakaowezesha mwanafunzi kurudi mkondo wa jumla kwa kujiunga na Kidato cha Tano au kuendelea na mafunzo ya Ufundi Sanifu bila kikwazo.
- Mwanafunzi katika mkondo huu anajifunza masomo ya fani yanayotolewa kwa kutumia mtaala wa VETA na kupimwa na NACTVET pamoja na masomo ya taaluma yanayotolewa kwa kutumia mtaala wa TET na kupimwa na Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA).
- Wanafunzi wa Mkondo wa Elimu ya Amali watafanya mitihani wa NACTVET wa umahiri kama ifuatavyo:
- Ngazi ya Kwanza (NVA I) mwishoni mwa Kidato cha Pili;
- Ngazi ya Pili (NVA II) mwishoni mwa Kidato cha Tatu; na
- Ngazi ya Tatu (NVA III) mwishoni mwa Kidato cha Nne.
- Mkondo wa Amali utahusisha masomo 4 ya lazima na na moja ya fani atakayochagua kutoka kwenye macahaguo
- Masomo manne (4) ya lazima ni yafuatayo:-
- Kiingereza(English)
- Hisabati (B/maths)
- Historia ya Tanzania na maadili
- Elimu ya biashara(business study)
- Shule yetu imekaguliwa na ina sifa za kutosha ikiwemo miundo mbinu vifaa vya kujifunzia na kufundishiua na mazingira mazuri ya kujifunza na kufundishia imepewa kibali cha kuanzisha mkondo wa Amali
- kibali cha mkondo wa Amali shuleni kwetu tumepewa fani zifuatazo:-
- masonry and bricklyaing
- electrical installation
- carpentry and joinery
- fitter mechanics
- solar power installation
- plumbing and pipe fitting
- graphic design
- computer programming
- welding and metal fabrication
- auto electric na
- designing sewing and cloth technology
- TUNAPENDA KUWAKARIBISHA WAZAZI WENYE WATOTO WANAOJIUNGA KIDATO CHA KWANZA MWAKA 2025 KUPATA ELIMU BORA YA KIAKILI,KIMWILI NA KIROHO PIA KWA MANUFAA YA WATOTO NA TAIFA KWA UJUMLA KARIBUNI SANA.
- ”ELIMU KWA WOTE NA WOTE KWA MUNGU”
