ABOUT US
HISTORIA YA SHULE
UTANGULIZI
Napenda kuushukuru uongozi wa Dayosisi mkoani Mara pale ulipokubali kujengwa kwa shule ya sekondari na ufundi Samaritan-Tarime, katika kikao cha mkutano mkuu (sinody) kilichokaa Mugumu May 2001 kupitia kamati ya mipango na maendeleo ya dayosisi-ilipopitishwa kujengwa shule hiyo. Shukrani za pekee pia ni kwa Baba Askofu Dr.Samson B.Mshemba -mkuu mstaafu wa K.K.K.T kwa kuweka wakfu eneo la ujenzi wa shule.
Hatua za Ujenzi na Kuanza kwa Masomo
- Ujenzi ulianza 2004-2008- majengo mawili yalikamilika na hapo Baba askofu Sospeter
Ndera Sagara aliyafungua majengo hayo tarehe 31.08.2008 - Tarehe 01-09-2008 Shule ilianza na wanafunzi saba (07) wa kidato cha kwanza.
- Shule ya sekondari ya ufundi Samaritan ilipata usajili na kupewa Na. S3884 toka wizara ya elimu na S.3906 toka baraza la mitihani.
- Shule ilisajiliwa kama ya Bweni na kutwa kwa mikondo miwili (02) kila darasa.
Shule ina mchepuo ya ufundi , sayansi na Sanaa kwa vidato vyote.
- Shule ipo katikati ya mji wa Tarime , mtaa wa Samaritan mkabala na Usharika wa K.K.K.T Tarime kati umbali wa Km 1 toka halmashauri ya mji wa Tarime.
